ZAIDI YA WAKAAZI ELFU 20 WAKOSA VITAMBULISHO TAITA TAVETA.


Zaidi ya watu 20,000 wakiwemo baadhi ya wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta wanaitaka serikali kuwatambua kama wakenya kwa kuwapa vitambulisho. 
 
Wananchi hao ambao baadhi yao ni wafanyikazi waliyostaafu wanasema hawajapata malipo yao ya kustaafu huku wengine wakosa kuajiriwa sawa na kunyimwa huduma mbalimbali muhimu kimaisha, kisa na maana ni kukosa stakabadhi mhimu ya kitambulisho cha kitaifa. 
 
Kwa sasa wanasema huenda ikawa vigumu kushiriki katika kura ya mwaka 2022 iwapo watakosa stakabadhi hiyo muhimu.