ZAIDI YA WAKAAZI 400 WADAI FIDIA,KUFUATIA ATHARI ZA UVAMIZI WA VIBOKO, MAGARINI KILIFI.


Jumla ya wakaazi 400 kutoka Sabaki kule eneo bunge la Magarini Kaunti ya Kilifi, sasa wanalalamikia kile walichokitaja kama kutolipwa fidia kufuatia athari za uvamizi wa viboko eneo hilo.

Wakaazi hao ambao wengi wao ni wakulima ,chini ya uongozi wa Sidi Mzungu Ndaa ,ambaye alipomteza mumewe miaka mitatu iliyopita kutokana viboko hao ,wanadai kuwa imekuwa vigumu kwao kupata fidia,huku mimea yao ikizidi kuharibiwa.

Naye Safari Kadenge ambaye ni mzee wa mtaa eneo la Moi kule Sabaki, amewasuta maafisa wa shirika la huduma za wanyama pori eneo hilo KWS ,kwa kukosa kuangazia swala hilo kwa wakati.

Wanadai kuwa Maisha yao yamo hatarini kwa sasa kutokana na kuzagaa kwa viboko hao, huku Afisaa wa shirika la KWS eneo la Malindi Jane Gitau ,akisema tayari majina ya waathiriwa hao yanashughulikiwa na afisi husika jijini Nairobi.