ZAIDI YA FAMILIA 85 ZAPATA CHAKULA CHA MSAADA LAMU.


Familia Zaidi ya 85 kisiwani Lamu kaunti ya Lamu zimepokea chakula cha msaada ikiwemo mchele, maharagwe na sukari kutoka kwa shirika la Anidan kisiwani humo .

Mariam Buu amelipongeza shirika hilo kwa msaada huo akisema kuwa familia nyingi zinakumbwa na changamoto ya kupata chakula kutokana na hali ngumu za kiuchumi kufuartia janga la korona.

Msimamizi wa shirika hilo Therashi Abdhallah  amesema  mpango huo ambao umegharimu takriban shilingi elfu 200 umefaidi familia ambazo hazina uwezo wa kupata chakula kutokana na kuathirika kwa shughuli zao za kiuchumi huku akitoa wito kwa  wadau mbalimbali kujitokeza zaidi ili kutoa msaada wa  chakula kwa wakaazi.