Yatima abakwa na mjomba Marigat, Baringo


Msichana wa miaka Kumi na sita analilia haki akidai kunajisiwa na mjomba aliyekuwa anakaa naye akiugua katika hospitali ya kimisheni ya Katoliki mjini Marigat kaunti ya Baringo.

Msichana huyo alikua amelazwa baada ya Kuchomwa kwa maji moto na pia alipatwa na Malaria.

Mjombake ambaye pia Ni mlezi wa msichana huyo yatima, aliwahadaa wahudumu wa hospitali hiyo kwamba msichana huyo alikuwa na kifafa na kuwa ni yeye tu angeweza kukaa naye akiwa amelazwa kwenye hospitali hiyo

Na hapo ndipo alimtendea unyama huo, ikiarifiwa kuwa sio mara ya kwanza kumdhalilisha kingono msichana huyo

Mshukiwa alikamatwa na kuachiliwa kwa njia isiyoeleweka, huku mkuu wa kituo cha polisi cha Marigat Benjoliv Munuve akikataa Kulizungumzia swala Hilo.