WITO WA UJENZI WA HOSPITALI MAENEO YA BONI , LAMU.


Mwakilishi wadi ya Hindi katika kaunti ya Lamu Anab Hajja ametoa wito kwa serikali kuu sawia na serikali ya kaunti kujenga hospitali katika maeneo ya Boni, ili kunusuru maisha ya wakaazi wa maeneo hayo.

Kulingana na Hajj kila mwezi katika maeneo hayo ya Boni,maeneo yaliyo ndani ya msitu wa Boni ,wanapoteza maisha ya mama au mtoto wakati wa kujifungua, ambapo hulazimika kusafiri umbali wa kilo mita zaidi ya 60 kupitia msitu huo ili kufika hospitalini.

Amesema walio ndani ya msitu wa Boni ni wakenya kama wakenya wengine ,na kwamba wanapaswa kupata huduma zinazohitajika kwani wao pia ni walipaji ushuru.