WITO KWA WANAFUNZI KUTOCHOMA SHULE- LAMU


Mkurugenzi wa elimu katika kaunti ya Lamu Joshua Kaaga, ametoa wito kwa wanafunzi wa shule ya upili ya wavulana ya Lamu ,kulinda shule yao badala ya kuiteketeza moto mara kwa mara.

Kaaga amesema mwaka 2018 shule hiyo ilichomwa moto zaidi ya mara tatu ,hali ambayo imetatiza pakubwa shughuli za masomo shuleni humo, ikizingatiwa kwamba shule hiyo ni miongoni mwa shule bora Lamu ,baada ya ile ya wavulana ya Mpeketoni.

Kulinganga na Kaaga vijana wengi wakiume wanaendelea kuangamia kutokana na maswala ya utumizi wa dawa za kulevya, sawia na uhalifu,hivyo basi wanapoendelea kuchoma shule zao ,elimu ya mtoto wa kiume itadorora.