Wezi wa nyaya za stima watiwa nguvuni Mombasa.


Maafisa wa usalama kule Changamwe Mombasa wamewatia nguvuni washukiwa saba waliofumaniwa wakiiba nyaya za umeme kwenye barabara kuu ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi.

Akizungumza wakati wa oparesheni hio naibu kamishana wa kaunti huko Changamwe Peter Sironka Ole-Masaa amesema kwamba saba hao wamefumaniwa na mirundo ya nyaya za stima aina ya Copper zinazopitishwa ardhini ambazo wamekuwa wakikata.