Wezi wa mifugo kupigwa risasi Laikipia


Mshirikishi mkuu wa serikali eneo l Rift valley George Natembeya ameagiza kupigwa risasi kwa wezi wa migugo kaunti ya Laikipia.

Anasema kuwa serikali kamwe haitavumilia wezi wa mifugo ambao wamekuwa wakitatiza amani nchini na hasa kaunti ya Laikipia.

Amesema haya katika mkutano wa amani kutokana na visa vya wizi wa mifugo Narasha lililo kati ya kaunti za Laikipia na Isiolo.

Natembeya aliyeandamana na viongozi na wakaazi kutoka jamii ya samburu na masai amehimiza wakuu wa jamii kusaidia katika kupatanisha jamii.

Licha ya hayo ameahidi kuongeza maafisa zaidi wa polisi wa akiba ili kuimarisha usalama eneo hilo.