WAZIRI WA FEDHA TANA RIVER MBELE YA KAMATI YA BUNGE,KUJITETEA KWA MCHAKATO WA KUMNG’ATUA.


Waziri wa Fedha kaunti ya Tana River, Mathew Babwoya, atalazimika kufika mbele ya kamati spesheli ya bunge la kaunti kujitetea baada ya wawakilishi wadi kuanza mchakato wa kumng’oa afisini.

Bunge limeidhinisha hoja ya kumng’atua mamlakani waziri huyo ,ambayo imewasilishwa na Naibu Kiongozi wa wengi, Salim Bonaya, kwa madai ya matumizi mabaya ya mamlaka, kukiuka katiba na kushindwa kutekeleza majukumu yake.

Kamati hiyo ya bunge ya watu watano itaongozwa na Ismail Kodobo, na inatarajiwa kumhoji waziri dhidi ya madai yaliyotolewa na kisha kuwasilisha ripoti kwa bunge kuidhinishwa au kuangushwa.