WAZIRI WA ARDHI TAITA TAVETA AZITAKA RANCHI KUFUATA SHERIA.


 

Waziri wa ardhi kaunti ya Taita Taveta Mwandawiro Mghanga, ameshikilia kwamba sharti mashamba makubwa yafuate sheria kwani mashamba hayo bado ni ya wananchi.

Mwandawiro anasema katika siku za hivi karibuni, watu wachache wameyafanya mashamba hayo kuwa ya kibinafsi ,jambo analolipinga zaidi.

Aidha Mwandawiro anasema sharti kuwe na uwazi katika suala zima la usimamizi wa mashamba hayo ,kwani mikataba baina ya wamiliki wa ardhi hizo na wafugaji inaenda kinyume cha sheria.