WAZIRI WA AFYA NCHINI YATAKIWA KUELEZE WAZI KUHUSU MATUMIZI YA FEDHA ZA KUPAMBANA NA CORONA.


Waziri wa afya nchini Mutahi Kagwe na ametakiwa kuwajibikia matatizo yanayokumba wizara yake kwa sasa kama vile kashfa ya kufujwa kwa fedha za kusambaza vifaa vya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Askofu wa kanisa la kianglikana dayosisi ya Taita Taveta Liverson Mng’oda amesema waziri huyo anapaswa kuwaelezea wananchi kile anachojua kuhusu kupotea kwa fedha hizo.

Askofu huyo ameongeza kuwa waziri Kagwe ana jukumu la kulinda mali ya uma dhidi ya waporaji.