Wazazi wakamatwa kutowapeleka watoto shule Tanariver.


Wazazi kumi kutoka vijiji vya Maroni, Hara na Gubani tarafa ya Wenje kaunti ya Tana River wakamatwa hii leo huku oparesheni kali ikianza dhidi ya wazazi ambao wamekaidi amri ya kupeleka wanafunzi waliomaliza darasa la nane mwaka jana shuleni kujiunga na kidato cha kwanza.

Oparesheni ambayo imeongozwa na Msaidizi wa Kamishna wa kaunti anayesimamia tarafa ya Wenje, Geoffrey Mwachofi imeanzia kijiji cha Hara ambapo wazazi saba wamekamatwa huku baadhi ya watoto ambao hawajaripoti shuleni ikibainika wamejiunga na shule za madrassa huku wengine wakisalia majumbani kuchunga mifugo..

Katika kijiji cha Maroni, wazazi wawili wamekatwa huku mmoja akiiamatwa katika kijiji cha Gubani huku msako ulitangazwa kote kaunti ya Tana River dhidi ya wazazi waliokaidi amri ya kupeleka watoto shuleni huku kaunti hiyo ikiorodheshwa ya mwisho kwa kuwa na idadi ndogo ya wanafunzi walioripoti kidato cha kwanza.

Waliokamatwa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Wenje huku machifu wakiwa na muda hadi siku ya ijumaa wiki hii kuhakikisha wanafunzi wote katika sehemu zao wameenda shule