WAZAZI WAJUKUMIKE VILIVYO TAITA TAVETA.


Wazazi katika kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kujukumika katika kushughulikia mahitaji ya watoto wao badala ya kuwatelekeza.

Afisa katika idara ya watoto kaunti ndogo ya Taveta Millecent Mchikirwa amesema idadi ya watoto wanaotelekezwa na wazazi wao imeongezeka zaidi katika kaunti hii.

Amesema kuwa changamoto za ukosefu wa kazi na gharama ya maisha kupanda hasa wakati huu wa janga la covid-19 zimepelekea wazazi wengi kutelekeza watoto huku wakikosa haki za kimsingi.