WAZAZI WAHIMIZWA KUWAHAMASISHA WATOTO WAO KUHUSU COVID 19 , MOMBASA.


Wazazi wametakiwa kuwaelimisha wanafunzi ambao wanaenda shuleni kwa sasa ,kuhusu umuhimu wa masharti ya kinga dhidi ya COVID 19, ikiwemo kuvaa barakoa, kuosha mikono miongoni mwa kanuni zengine, ili waweze kutambua kuhusu ugonjwa huo.

Ni kupitia njia hii ambapo watoto hao wataweza kuishi kwa urahisi ,wakizingatia umuhimu wa mikakati hiyo bila kushurutishwa.

Kulingana na mshirikishi mkuu kanda ya Pwani John Elungata ,hamasa hiyo itarahisisha maisha ya wanafunzi hao wanapokuwa shuleni kila mara.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kujifunza kutokana na kufungwa kwa muda kwa shule mbili hapa mjini Mombasa ,kufuatia kuripotiwa kwa virusi vya corona katika shule hizo, huku akiongeza kwamba tayari wanafunzi wamepoteza miezi mingi kukosa elimu hivyo basi ni sharti kila mmoja awe makini.