WAZAZI LAMU WATAKIWA KUTIMIZA MALENGO YA WATOTO WAO KWA KUJUKUMIKA .


Wito umetolewa kwa wazazi wa kaunti ya Lamu kujukumika ipasavyo na kuwasaidia wanawao ili kufikia na kufanikisha  malengo yao yatakayowasaidia kupata ajira siku za mbeleni.

Mwakilishi maalum Lamu Fatma Salim amesema vijana wengi kaunti ya Lamu wamekosa kuendeleza na kukamilisha masomo yao baada ya kukosa huduma za kimsingi kutoka kwa wazazi wao.

Salim ametaka wamama na mababa wote kuwajibikia swala hilo kwani vijana ndio viongozi wa siku za mbeleni katika taifa hili.