Wawili waaga kufuatia ajali katika eneo la Komaza Kilifi


Polisi mjini Kilifi wanachunguza kisa ambapo Watu wawili wamefariki katika ajali mbaya eneo la Komaza kule kaunti ya Kilifi.

Kulingana na kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi steven Mathu ajali hiyo ilihusisha boda boda la lori.

Matu anahoji kuwa mwendeshaji pikipiki alikuwa akijaribu kupita lori hilo kabla ya kuingia chini yake na hatimaye kuangamia.

Inaarifiwa kuwa pikipiki hiyo ilikuwa ikiendeshwa kuelekea majajani wakati ajali hiyo ilipotokea.

Taarifa zimefichua kuwa mwendeshaji Pamoja na abiria wake wamepoteza uhai papo hapo baada ya lori hilo kupita juu yao.

Kulingana na matu abiria katika ajali hiyo alikuwa mmoja wa maafisa wa elimu mjini Kilifi.

Matu amewataka wahudumu wa pikipiki kuwa makini zaidi wakati wanapohudumu katika barabara.

Maiti za wawili hao zinahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya kaunti mjini Kilifi.