Wavuvi 3 wapotea Ziwa Victoria


Wavuvi katika fukwe za Ngore Nyatike kaunti ya Migori wanaitaka serikali kuwasaidia kuwatafuta wenzao watatu wanaoarifiwa kupotea Ziwa Victoria tarehe 29 mwezi uliopita .

Mwenyekiti wa usimamizi wa fukwe hizo Orem Sobu ameambia radio Citizen kuwa wamekuwa wakiwatafuta wavuvi hao lakini juhudi zao hazijazaa matunda akihofia huenda walizama ndani ya ziwa.

Anasema kuwa wavuvi hao walienda ziwani kuvua samaki tarehe 29 mwezi Julai lakini hawakurejea, mashua yao ikipatikana tarehe 31 mwezi uo huo katika ufuo wa Ndhiwa kaunti jirani ya Homabay bila yeyote.