Wauzaji bidhaa waonya dhidi ya kuongeza bei


Mamlaka ya kuangazia ushindani nchini imeonya watengnezaji bidhaa au wauzaji dhidi ya kuongeza bei ya bidhaa hasa wakati huu ambapo Kenya imethibitisha kisa cha kwanza cha virusi vya Corona.

Mamlaka hiyo inasema kuwa washukiwa watatozwa faini kali ikiwemo asilimia 10 ya pato lao.

Ni hatua inayojiri huku idadi kubwa ya wakenya ikishuhudiwa katika maduka mengi ya jumla kununua bidhaa mbalimbali.

Yakijiri hayo, Mamlaka ya kuthibiti bima nchini imewahakiksihia wakenya kuwa bima ya afya itagharamia matibabu ya ugonjwa wa Covid-19.

Katika taarifa, mamlaka hiyo imesema kuwa tayari imefanya mazungumzo na wamiliki wa bima nchini na kuafikiana hilo.