Wauguzi kaunti ya Mombasa watoa ilani ya Mgomo.


Wauguzi katika kaunti ya Mombasa wamepeana makataa ya siku 7 kufanya mgomo kutokana na mazingira duni ya kufanya kazi.

Wakiongozwa na katibu wa muungano wa chama cha wauguzi tawi la Mombasa Peter Maroko, wauguzi hao wamesema kuwa wamekuwa wakifanya kazi huku wakiwa katika hatari ya kupata ugonjwa wa COVID-19.