Watumizi wa kivuko cha feri kufunika pua na mdomo kabla kuvuka.


Wananchi wote wanaotumia kivuko cha Likoni Ferry watalazimika kuanzia leo sasa kufunika midomo na pua zao kutumia vitambaa au chochote kile kabla ya kabla ya kuabiri ferry hizo.

Haya ni kwa mujibu wa kamati inayodhibiti kuenea kwa virusi vya korona ikiongozwa na kamishna wa kaunti ya mombasa Gilbert Kitiyo ambayo pia imeamuru kwamba wananchi wote walio na dalili za ugonjwa wa mafua kutoabiri ferry bali watafute huduma za matibabu.

Aidha kamishna wa kaunti ya Mombasa Gilbert Kitiyo amewataka wote wasio na shughli za kwenda mjini kusalia majumbani na pia kuwataka wafanyibiashara wa bidhaa za jumla mombasa kutii agizo la kuhama na kuelekea awlikotengewa.