Watu wenye vimo vifupi Pwani walalamikia kutengwa.


Baadhi ya watu wenye vimo vifupi wanasema kwamba hawakuridhishwa na jinsi zoezi la sensa lilivyotekelezwa, kwani baadhi yao hawakuorodheshwa kwenye kundi la walemavu.

Wakizungumza katika hafla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa kuhusu watu wenye vimo vifupi, iliyoandaliwa katika eneo la Rabai kaunti ya kilifi, watu hawa wamesema kuwa iadadi yao kamili haijabainika wazi huku wakisema baadhi ya maswali waliyoulizwa hayakuwazingatia.