WATU WAWILI WAFARIKI KATIKA AJALI-MWATATE


Mwendesha bodaboda na abiria wake ambaye ni mama wamefariki papo hapo baada ya kuhusika katika ajali mbaya ya barabara katika eneo la Mto wa Mwagodi barabara ya Voi kuelekea Mwatate.
Wawili hao wameangamia baada ya kugongana ana kwa ana na gari la serikali liliokua likielekea upande wa Mwatate kugongana na pikipiki hiyo ambayo ilikua ikielekea upande wa Voi.
Kwa sasa mtoto ambaye alikua amebebwa na mamake wakati wa ajali hiyo amekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi.