Watu watano wafa maji mto Nzoia, eneo la Ugunja


Watu watano wamekufa maji katika mto Nzoia baada ya boti waliyokuwa wakitumia kwa usafiri kuzama karibu na eneo la Sango-Umala huko Ugunja kaunti ya Siaya

Watu wengine wanne walinusurika kifo katika mkasa huo wa alasiri

Walioshuhudia mksasa huo wameiambia Radio Citizen kuwa boti hiyo ilikuwa imekodishwa kutoka Budalangi, kaunti ya Busia ili kusaidia juhudi za kutafuta maiti ya mtu aliyekuwa amezama katika mto huo wa Nzoai hapo jana

Aidha wamesema baada ya shughuli ya kuutafuta mwili huo kuonekana kutozaa matunda, watu hao tisa wakaiabiri boti hiyo kwa lengo la kufikishwa Sango-Umala, na ndipo injini yake ikafeli na hivyo kuzama

Naibu kamishna wa Siaya Joseph Sawe anasema shughuli ya kutafuta maiti za wahasiriwa imeanzishwa