Watu 9 waaga dunia katika ajali Kilifi


Watu 9 wamefariki dunia papo hapo baada ya ajali mbaya iliyohusisha matatu na lori kutokea katika barabara kuu ya Mazeras – Kaloleni kaunti ya Kilifi.

Kulinganga na kamanda wa polisi kaunti ya kilifi Steven Matu, magari hayo yaligongana ana Kwa ana kabla ya kusababisha vifo vya watu hao miongoni mwao watoto wawili.

Hata hivyo amesema kuwa madereva wa magari hayo wamenusurika katika ajali hiyo.

Matu amewataka wananchi na watumizi wa barabara kuwa makini hususan wakati huu wa kukaribia msimu wa sikukuu ya krismasi na mwaka mpya.