Watu 89 wakamatwa Nakuru kwa kupuuza masharti ya kuzuia Corona


Watu 86 wamekamatwa mjini Nakuru kwa madai ya ukiukaji wa sheria zilizowekwa na wizara ya afya kuzuia virusi vya corona.

Wengi wa waliokamatwa walitiwa mbaroni katika vilabu vya uuzaji pombewakati wa kafiu.

Kwa mujibu wa afisa mkuu wa polisi eneo hilo, waliokamatwa wengi wao ni vijana na kutoa onyo kali kwa wanaokiuka sheria za serikali.

Polisi wamesema kuwa hawatalegeza kamba katika kuhakikisha kuwa sheria za kuthibiti Covid 19 ilivyotangaza serikali zinazingatiwa.