Watu 5 wauawa kaunti ya Wajir


Watu watano wameuawa huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya katika mapigano ya kiukoo katika eneo la Bute, eneo bunge la Wajir Kaskazini kaunti ya Wajir.

Kamanda wa polisi  eneo la kaskazini Mashariki mwa nchi  Rono Bunei anasema uhasama huo unahusisha makundi mawili katika ukoo wa Arjuran na ule wa Konso.

Maafisa wakuu wa usalama wamezuru eneo hilo kupatanisha pande hizo mbili.