Watu 3 waaga katika ajali Taita Taveta.


Watu watatu wamefariki asubuhi ya leo baada ya gari aina ya canter iliyokua imebeba mahindi kugongana na lori la kubeba Mogokaa katika makutano ya barabara ya Voi – Mwatate na Nairobi – Mombasa kaunti ya Taita Taveta.

Watatu hao walifariki papo hapo huku wengine wawili waliopata majeraha wakipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kwa matibabu zaidi.