Watu 2 wauawa kinyama kaunti ya Isiolo


ISIOLO DEATHS

Wingu la  simazi limetanda katika kijiji cha Rapso kaunti ya Isiolo baada ya wanaume wawili kuuawa na  watu wanaodaiwa kutoka kaunti jirani ya Garissa.

Wawili hao walikuwa wamewapeleka mifugo wao   kwa malisho  katika eneo hilo.

Wakazi wanasema kuwa mmoja Wa waliouawa ni Kijana Wa miaka 22 na huyo mwingine ni Mzee Wa miaka 66.

Wakaazi wanasema kuwa kitendo hicho si cha kwanza, kwani mwezi uliopita watu wengine wawili waliuawa eneo hilo.

Aidha wanaitaka serikali kuu kupitia maafisa wa usalama kuchukua  hatua na kuwakabili  wavamizi hao.

Waliofariki dunia wamezikwa leo kufuatia kanuni za dini ya kiislamu.