Watu 2 wafariki katika ajali Makueni


Watu wawili wamedhibitishwa kufariki huku wengine wawili wakijeruhiwa kufuatia ajali iliyohusisha lori na trela katika eneo la ACK kati ya mji wa Salama na Malili barabara ya Mombasa- Nairobi kaunti ya Makueni.

Kaimu kamanda wa polisi Makueni Justus Kitetu anasema kuwa ajali hiyo hiyo ya usiku wa kumkia leo ilisababishwa na trela hilo lililokuwa likipita magari mengine likielekea Mombasa na kugongana ana kwa ana na lori hilo wawili hao ambao ni wanawake wakiaga papo hapo.

Madereva wote wawili walinusurika na majeraha.

Mili ya wawili hao inahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Machakos uchunguzi zaidi ukifanywa.