Watu 15 wafariki katika ajali ya barabarani eneo la Kizingo Malindi.


Watu 15 wamefariki huku wengi wakijeruhiwa baada ya ajali mbaya kutokea katika eneo la Kwashume kule Kizingo Malindi kaunti ya Kilifi.

Kulingana na Kamishena wa kaunti ya Kilifi Kutswa Olaka ajali hiyo ilihusisha basi la Muhsin ambalo lilikuwa likelekea Garisa kutoka Mombasa ambalo liligongana ana kwa ana na lile la Sabaki Travelers Sacco ambalo lilikuwa likitoka Malindi kulekea Mombasa.

Olaka amedokeza kuwa basi la Muhsin lilipoteza mwelekeo baada ya mguu wake kupasuka na kugongana ana kwa ana na Basi la Travelers Sacco.

Hata hivyo Olaka amefichua kuwa hajaridhishwa na mwanakandarasi anayejenga barabara ya Malindi Mombasa ambaye amechimba barabara hiyo na kuiacha.

Alikuwa ameasndanamana na kamanda wa polisi kaunti ya Kilifi Nelson Tiliti ambaye ameonya wakaazi dhidi ya kuiba badala ya kuokoa.