Watu 10 waaga dunia kutokana na Covid-19


Visa vipya 780 vya virusi vya corona vimedhibitishwa nchini baada ya watu 6,158 kupimwa na kuongeza jumla ya walioambukizwa virusi hivyo  kufika 80,102.

Kupitia ujumbe kwa vyombo vya habari waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha vifo vya watu 10 katika kipindi cha saa 24 kutokana na virusi hivyo , na kuongeza jumla ya idadi ya waliopoteza maisha kufikia 1,427.

Aidha  watu 552 wamepona virusi hivyo japo kuna wengine 7, 295 ambao wamejitenga nyumbani.

Kadhalika kuna watu wengine 57 ambao wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.

Kaunti ya Nairobi inazidi kuongoza katika kunakili visa vingi hii leo ikiwa na visa 273, Kiambu 93 Mombasa 85 Busia nayo ikiwa na visa 85.