Watu 10 waaga dunia kutokana na Covid-19


Idadi ya watu walioambukizwa virusi vya corona nchini imeongezeka hadi 92, 853 baada ya visa vipya 394 kudhibitishwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita..

Kwa mujibu wa waziri wa afya Mutahi Kagwe watu wengine 10 wameaga dunia  kutokana na virusi hivyo jumla ya walioaga dunia kufikia kutokana na virusi hivyo kote nchini kufikia sasa ikiwa 1,614.

Aidha watu 424  wamepona Covid-19  japo, 810  wangali wamelazwa katika vituo tofauti vya afya 46 kati yao wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.