WATATU WATIWA MBARONI KUTOKANA NA KISA CHA UBAKAJI LAMU.


Watu watatu wametiwa mbaroni na maafisa wa polisi eneo la Mpeketoni kufuatia kisa cha ubakaji ,alichotendewa msichana mwenye umri wa miaka 14, kilichotokea eneo la Bomani Mpeketoni kaunti ya Lamu.

Mnamo Mwezi Januray mwaka huu, msichana huyo darasa la tatu alivamiwa na babake chumbani kwake na kumbaka , kisha kaka ya babake naye akamfanyia tena kitendo hicho cha unyama .

Msichana huyo alikuwa akiishi kwa nyanyake na baada ya kisa hicho ,alihamishwa yeye pamoja na dadake mkubwa umri wa miaka 16 kupata hifadhi kwa mamake mdogo eneo la Shee Mgambo Hindi kaunti hiyo.

Watatu hao waliokamatwa kutokana na kisa hicho ,ni baba ya mshukiwa wa ubakaji, kaka ya baba huyo sawia na nyanya aliyekuwa akiishi na msichana huyo eneo hilo la Bomani.

Inaarifiwa kwamba mwanamume huyo kwa jina David Muthui umri wa miaka 45 ,alipata virusi vya ukimwi kutoka kwa mke wake mdogo aliyefariki ,ambaye alimuoa baada ya kuachana na mama ya msichana huyo ,lakini bado haijabainika iwapo ni yeye ndiye aliyempachika mwanawe virusi vya ukimwi.