WATANO WAJERUHIWA KWENYE AJALI KULE JOMVU MOMBASA


Wasafiri watano miongoni mwao abiria wanne na dereva mmoja wamejeruhiwa baada ya gari walimokuwa wakisafiria aina ya matatu kuhusika kwenye ajali katika barabara kuu ya kutoka Mombasa kuelekea Nairobi katika eneo la Jomvu Mombasa.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho matatu ya abiria iliyokuwa inatoka Mombasa kuelekea sehemu ya Miritini iligonga kighafla lori aina trela iliyokuwa imepunguza mwendo ilikupinda katika sehemu ya EPZ Kingorani.

Naibu Afisa mkuu wa polisi katika eneo la Jomvu Joseph Odhiambo amedhibitisha kisa hicho na kusema kwamba waliojeruhiwa wamekimbizwa katika hospitali tofauti ilikupokea matibabu  huku uchunguzi ukianzishwa kubaini kilichochangia ajali hio.

Haya yanajiri huku wito ukitolewa kwa madereva wanaotumia barabara hio kuwa makini na hasaa kwa wakati huu ambao ujenzi wa barabara hiyo ungali unaendelea.