Watakaopata alama 300 na zaidi kufadhiliwa Lamu.


Gavana wa kaunti ya Lamu Fahim Yasin Twaha amewahakikisha wanafunzi wote wa Lamu ambao watapata alama Zaidi ya 300  kwamba wataendeleza masomo yao pasipo kulipa karo shuleni.

Kulingana na Twaha serikali ya kaunti ya Lamu inawafadhili wanafunzi wote kikamilifu ambao watapata alama Zaidi ya 300 na mzazi anachotakikana kununua ni vitabu,sare za shule na vifaa vyenginevyo vya shule.

Akizungumza na baadhi ya wanafunzi gavana Twaha amesema pia wanafunzi wanapomaliza kidato cha nne serikali ya kitaifa itawapa mikopo ya kujiendeleza HELB.