Wasichana 5,000 wapachikwa mimba Siaya


Kamishna wa kaunti ya Siaya Michael Ole Tialal anasema kuwa kaunti hiyo imerekodi zaidi ya visa 5,000 vya mimba za mapema miongoni mwa wasichana wadogo tangu mwezi Januari mwaka huu.

Ole Tialal anasema data zainaonyesha kwamba wasichana 310 walio na kati ya umri wa miaka 10 na 15 walipachikwa mimba tangu mwezi januari hadi Mei mwaka huu huku wengine 3,200 wa umri wa kati ya miaka 15 na 16 wakipachikwa mimba katika mudauo huo.

Idadi hiyo sasa anasema imeongezeka na kufikia 5,000

Ole Tialal ameelezea wasiwasi kuwa huenda hali hiyo iawa na athari kubwa kwa kaunti hiyo hivi karibuni hasa kuhusiana na elimu.

Amewaonya wanaotekeleza uovu huo dhidi ya watoto wakiwemo wazazi ambao wamekuwa wakiwasitiri washukiwa.