Washukiwa wa shambulizi la kigaidi Westgate kuhukumiwa leo


Washukiwa watatu waliopatikana na hatia ya kuhusika katika shambulizi la kigaidi katika jumba la kibiashara la Westgate mwaka 2013 wanatarajiwa kuhukumiwa leo

Hakimu wa mahakama ya Nairobi Francis Andayi aliahirisha utoaji hukumu hiyo tarehe 18 mwezi uliopita wa Septemba hadi leo

Watuhumiwa hao watatu, Mohammed Ahmed Abdi, Liban Abdullahi, na Hussein Hassan Mustafa walipatikana na hatia ya kuwa nchini kinyume cha sheria, kuwa wanachama wa kundi la kigaidi na kuhusika katika shambulizi la kigaidi katika jumba hilo la kibiashara

Watu 67 waliuawa huku wengine 150 wakijeruhiwa baada ya shambulizi hilo la jumamosi tarehe 21 mwezi Septemba mwaka 2013, mtaani Westlands hapa Nairobi