Washukiwa 2 wa ujambazi wauawa Mombasa


Maafisa wa polisi mjini Mombasa wamewaua washukiwa wawili wa ujambazi kwa kuwapiga risasi katika eneo la Minalove kule Mshomoroni Kisauni Mombasa.

Kulingana na afisa mkuu wa polisi Kisauni Julius Kiragu, wawili hao waliokuwa wakitumia pikipiki waliandamwa na maafisa wa polisi kwa tuhma za kutekeleza ujambazi na hasaa kuwaibia wahudumu wa maduka ya Mpesa Mombasa.

Kiragu amesema kwamba polisi wamefanikiwa kupata bastola moja aina ya Seska iliokuwa inatumiwa na washukiwa hao na wanafanya msako wa washukiwa wengine wanaodaiwa kush