Washiali kueleza ni kwa nini wanafunzi wanaogelea kwenda shule-Mahakama


Mahakama mjini mumias kakamega imeagiza maafisa katika serikali kuu na ile ya kaunti, mbunge wa mumias mashariki Benjamin Washiali na mwakilishi wadi wa malaha makunga isongo kufika mbele ya mahakamak hiyo kuelezea hatua waliochukua kuhusu wanafunzi walioripotiwa na Radio Citizen kuogelea wakielekea shuleni.

Hakimu mkuu mwandamizi katika mahakama hiyo teresa odera amesema kuwa agizo hilo linatolewa kwa manufaa ya wanafunzi hao ambao wanakabiliwa na changamoto tele kufika shuleni.

Kesi hiyo ilipelekwa mahakamani na shirika linalopigania haki la Torch Afrika.

Kesi hiyo itasikizwa tarehe 27 mwezi huu

Haya yakijiri wenyeji katika eneo la petros na nyaporo walifanya kikao na kuchagua kamati itakayosimamia ujenzi wa daraja la muda huku wakisubiri kaunti kuwajibika na kuwajengea daraja la kudumu.