Wanawake na uvyeti vya umiliki ardhi.


Wananchi kutoka maeneo ya kishushe kaunti ndogo ya Wundanyi kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kujitokeza kwa wingi kwa zoezi linaloendelea la kupimwa mashamba ili kupewa vyeti vya kumiliki ardhi.

Kulingana na naibu kamishna eneo hilo Victor Kisachi maafisa hao wamekuwa hapo kwa mda wa mwezi mmoja na jukumu kubwa nikuhakikisha maafisa hao wanasikiza kesi za ardhi zilizoko maeneo hayo ambapo wengi wanalalamikia kupokonywa ardhi zao.

Kisachi ameongeza kuwa wananchi wote walio tuma malalamishi yao watasaidiwa na kuhakikisha wanapata vyeti vyao kwa njia inayo stahili.