Wanawake kuboresha uchumi wao Tanariver.


Wanawake kaunti ya Tana River wahimizwa kuchukua fursa mbalimbali za kuboresha uchumi ambazo zimetolewa maalum kwa ajili ya wanawake nchini na serikali ya kitaifa ili kujikimu kimaisha.

Waziri wa Elimu, Jinsia, vijana na michezo kaunti ya Tana River, Abbas Kunyo, anasema ili kuhakikisha jinsia ya kike inapewa fursa sawa kama wanaume, serikali imeamzisha hazina mbalimbali ikiwemo ile ya Women Enterprise Fund sawia na sawia na sheria ya asilimia 30 ya zabuni kupewa wanawake, vijana na walemavu ili kuwasaidia kiuchumi.

Akiongea katika hafla ya wanawake mjini Hola, Waziri huyo anasema swala la jinsia linafaa kuboreshwa katika wizara zote za serikali ya kitaifa, zile za kaunti na hata mashirika huku kukiwa bado kuna lalama kwamba wanaotuma maombi kutafuta fedha katika hazina za mkopo unaotolewa na serikali kwa makundi maalum kama wanawake bado iko chini eneo hilo.