WANASIASA WACHOCHEZI MITANDAONI WAONYWA,KWALE.


Tume ya uwiano na utengamano wa taifa NCIC ,imetakiwa kuwachunguza viongozi wanaoeneza siasa za uchochezi katika mitandao ya kijamii kaunti ya Kwale.

Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la kutetea haki za kibinadamu la HURIA Yusuf Lule ,amesema tayari wameliwasilisha suala hilo kwa tume ya NCIC wakiitaka iwachunguze viongozi ,wanaowachochea wakaazi katika kampeni za uchaguzi mdogo wa Msambweni.

Kando na hayo Lule amesema kuwa shirika hilo linafuatilia jinsi wagombea wa kiti cha ubunge wa Msambweni ,wanavyoendesha kampeni zao kwa kuzingatia masharti ya kukinga wananchi dhidi ya ugonjwa wa corona ,ikizingatiwa wengi wanaendelea na mikutano hiyo.