Wanaoaga dunia Nairobi wazikwe Nairobi- Raila


Kinara wa ODM Raila Odinga amehimiza wakenya kuzingatia maagizo ya serikali ili kuzuia maambukizi ya virusi vya Corona.

Raila amepuzilia mbali wanaoshinikiza shughuli za taifa kufungwa kote nchini ili kuzuia maambukizi zaidi akisema huenda hilo likawa na athari za kiuchumi.

Akizungumza na Ramogi Fm mojawapo ya vituo vinavyomilikiwa na kampuni ya Royal Media, Raila ameshabikia mpango wa serikali wa kupima halaiki kubaini iwapo wana virusi vya corona au la kwa misingi kuwa hiyo ndiyo njia pekee itakayotoa uhalisia wa mambo kuhusu ugonjwa wa Covid-19.

Raila aidha ameelezea haja ya mili ya wanaoaga dunia hapa Nairobi kuzikwa hapa kuliko kusafirisha hadi maeneo ya mashinani katika juhudi za kuzuia maambukizi zaidi ya virusi vya Corona.