WANANCHI WAKABILI VIRUSI VYA CORONA, TAITA TAVETA.


Changamoto imetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta kufuata maagizo ya wizara ya afya ,ili kupunguza idadi ya wanaoambukizwa virusi vya Corona.

Kulingana na gavana wa kaunti hiyo Granton Samboja anasema, mji wa Voi hivi punde umeathirika zaidi na maambukizi ya virusi vya Corona, huku akisema serikali ya kaunti itashirikiana na maafisa wa usalama, ili kuwakabili wasiofuata maagizo hayo.

Samboja wakati huo anasema hata baada ya serikali kujitayarisha kukabili virusi hivyo, ni sharti wananchi wawe katika mstari wa mbele kukabili virusi hivyo.