WANANCHI WAHAMASISHWE KUHUSU ARDHI KAUNTI YA TAITA TAVETA.


Kuna haja kwa jamii kuhamasishwa kuhusu sheria za ardhi kwani wengi hawana ufahamu kamili hali inayosababisha mizozo ya mara kwa mara baina ya wanajamii.

Kulingana na afisa wa usajili wa ardhi kaunti ya Taita Taveta Michael Siego anasema kukosekana kwa ufahamu kuhusu ardhi ya jamii kumesababisha wananchi kukosana kila mara hasa maeneo ya mashinani.
 
Siego akitoa wito kwa wadau katika sekta ya ardhi kufanya hamasisho kwa wananchi kuhusu suala la ardhi sawa na kuhusisha jamii moja kwa moja.