WANANCHI WACHANGIE UTOAJI DAMU,TAITA TAVETA


Changamoto imetolewa kwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta kujitokeza na kutoa damu hasa inapohitajika.

Kulingana na muungano wa maafisa wa afya ya nyanjani wanasema kaunti hiyo inakabiliwa na ukosefu wa damu mara kwa mara hasa kutokana na ajali zinazotokea katika barabara kuu ya Nairobi Mombasa.
Aidha wanasema iwapo wananchi watajitolea kikamilifu huenda ikasaidia hata kaunti jirani ambako visa vya ajali vinashuhudiwa mara kwa mara.