Wanamgambo 3 wa Alshabab wauawa


Kikosi maalum cha wanajeshi, kimefanikiwa kuwauwa kwa kuwapiga risasi washukiwa watatu wa kundi la kigaidi la Al Shabaab katika msitu wa Boni, Lamu

Aidha wanajeshi hao walifanikiwa kumkamata mmoja, walipovamia kambi yao karibu na eneo la Bothia huko Lamu

Wanajeshi hao wanatoa ulinzi kwa wakazi wa lamu hasa wanaopakana na msitu huo wa Boni, u naoaminika kuwa maficho ya wanamgambo hao wa kutoka taifa jirani la Somalia