WANAFUNZI WOTE WARUDI SHULENI ASEMA MAGOHA.


Waziri wa Elimu Prof.George Magoha ametoa changamoto kwa wazazi kwamba ,wanafunzi wa kike ambao wamejifungua wakiwa nyumbani msimu huu wa janga la Covid-19, lazima warudi Shuleni kusoma.

Akihutubia Wanahabari katika maeneo ya Kapsabet baada ya kukagua Maktaba ya Kisasa , Magoha anasema Serikali kupitia wizara ya usalama wa Ndani , itatumia Wasimamizi wa Mikoa kuhakikisha kuwa wanafunzi ambao waliolewa , lazima warudishwe shuleni pamoja na wenzao.

Magoha aidha amesema Wizara ya elimu inafanya kila iwezavyo , ili kuona kwamba wanafunzi wote wanafanikiwa katika masuala ya elimu ,na kuongeza kuwa kwa sasa Wizara yake iko mbioni kushughulikia maswala ya madawati ,ili kuwawezesha wanafunzi kufuata masharti ya umbali wa mita moja ndani na nje ya madarasa.