WANAFUNZI WAONYWA, TAITA TAVETA.


Wamiliki wa maeneo ya burudani na wazazi kaunti ya Taita Taveta wameshauriwa kuwazuia wana Wao na wote walio chini ya umri wa miaka 18 ,dhidi ya kujihusisha na starehe zisizofaa msimu huu ambapo wanafunzi wako nyumbani.

Kulingana na mwanaharakati Frida Mwangemi anasema ,visa ambapo wanafunzi wanajihusisha na starehe zisizo na msingi haswa wakati huu vimeongezeka, huku matokeo yake ikiwa ni mimba za mapema kwa wasichana wadogo.

Hata hivyo umaskini sawia na uzembe wa baadhi ya wazazi ,umetajwa kuwa mojawapo wa sababu kuu za wasichana wadogo kujihusisha na starehe zisizo na msingi , ikiwemo uchangudoa hasa majira ya mchana peupe.