WANAFUNZI WA VOI KURUDI SHULENI JUMATATU, BAADA YA SHULE HIYO KUFUNGWA KWA MAJUMA MAWILI


Wanafunzi katika shule ya msingi ya Voi kaunti ya Taita Taveta iliyofungwa majuma mawili yaliyopita, baada ya waalimu watatu kuambukizwa virusi vya Corona,wanatarajiwa kufunguwa upya na kuripoti shuleni, jumatatu juma lijalo.

Kulingana na mwenyekiti wa shule hiyo ,ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha wazazi kaunti ya Taita Taveta Elias Mberi ,anasema shule hiyo imeweka mikakati ya kutosha kuhakikisha masomo yanarejelewa siku hiyo.

Mberi aidha amesema waalimu wote 40 wa shule hiyo, wamepimwa na kwamba hawana virusi vya Corona.